Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:03

Kamala Harris huenda akateuliwa kushika wadhifa wa juu katika chama cha Democratic


Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris

Kamala Harris, mwanamke wa kwanza kuwahi kuwa makamu rais huenda akateuliwa kushika wadhifa wa juu kwa chama cha Democratic kuwania urais wa Marekani.

Mwandishi wa VOA Carlyn Presutti anaangalia nyuma alikotokea na miaka minne ambayo amekuwa katika uongozi wa juu.

Ilikuwa ni wakati wa kutengeneza historia nchini Marekani mwaka 2021…... ……wakati Seneta wa zamani Kamala Harris alikuwa ni mwanamke wa kwanza kuwa makamu rais katika taifa la Marekani.

Kamala Harris, Makamu Rais, Marekani alieleza: “Ni heshima kubwa kwa mimi kuwa hapa, kusimama bega kwa began a wale ambao walikuja kabla yangu.”

Harris pia ni mwanamke wa kwanza Mmarekani Mweusi na Mmarekani mwenye asili ya India kulihudumia taifa katika nafasi ya pili ya juu katika taifa.

Mwakilishi Barbara Lee, Mdemocrat anaeleza: “Amevunja vioo vingi katika dari kwa ajili ya wanawake wengi.”

Mtoto wa mama mhindi na baba mwenye asili ya Jamaica, Harris alizaliwa Oakland, California. Picha yake ilionekana kwenye shule ambayo alikuwa akienda alipokuwa mtoto…..kama sehemu ya juhudi za muingiliano kwa watu wa rangi tofauti.

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Howard, Harris amekuwa mwanamke wa kwanza mwanasheria wa serikali huko San Franscisco mwaka 2004, na halafu mwaka 2011, mwanamke wa kwanza mweusi kuhudumu kama mwanasheria mkuu wa California.

Katika miaka yake kama makamu rais, Harris amekuwa anaongelea sana kuhusu Mahakama ya Juu Marekani kubadili uamuzi wa mwaka 1973 katika kesi ya Roe vs Wade ambayo ilifanya utoaji mimba kuwa halali kote nchini. Wakati wa uongozi wake, Rais wa zamani Donald Trump aliwateua majaji watatu waconservative kwenye Mahakama ya juu.

Kamala Harris, Makamu Rais, Marekani alisema: “Kwa fahari, anatumia neno fahari, anachukua sifa kwa kubadili uamuzi wa Roe vs Wade kuhusu utoaji mimba, kwahiyo msifanye kosa – kama Trump akipata fursa, atatia saini kupiga marufuku utoaji mimba kitaifa na kupiga marufuku utoaji mimba katika kila jimbo.”

Makamu wa Rais Kamala Harris
Makamu wa Rais Kamala Harris

Makamu rais pia alipongeza kuendeleza kwa Sheria ya Huduma za Afya na kupunguzwa kwa bei ya dawa kisukari hatua iliyofanikishwa na utawala wa Biden.

“Nyoosha mkono wako kama una mwanafamia ambaye ana kisukari.”

Mwanzoni kabisa, alitajwa kuongoza juhudi za utawala katika mpaka. Lakini kampeni ya Biden iliishia kujitetea, huku suala kuu la uhamiaji likiwa katika uchaguzi wa mwaka huu.

Kamala Harris, Makamu Rais, Marekani anasema: “Hivi sasa, washirika wasio na nyaraka halali wenye uhusiano na raia wa Marekani ambao wamekuwa humu nchini kwa miaka kumi au zaidi wanaweza kubaki katika nchi wakati wakiomba kupatiwa kadi ya kijani.”

Akiongea na makundi yanayounga mkono uhamiaji kama Wamarekani wenye asili ya Asia, Wazawa wa Hawaii na wakazi wa kisiwa cha Pacific, haraka aligeuza lengo kwa maneno ya Donald Trump.

Kamala Harris, Makamu Rais, Marekani anaeleza: “Kwa mtu ambaye anawachafua wahamiaji, ambaye anahamasisha kuwachukia wageni, mtu ambaye anaonyesha chuki kamwe asipewe fursa ya kusimama nyuma ya kipaza sauti na kuwa na muhuri wa Rais wa Marekani.”

Harris amekuwa akijitokeza sana katika mikutano ya ksiiasa kama hii ya kwenye kampeni, baada ya Rais Joe Biden kutofanya vizuri katika mdahalo wa mwezi Juni na Rais wa zamani Donald Trump.

Kamala Harris, Makamu Rais, Marekani anaeleza: “Tulimshinda Trump mara ya kwanza na tutamshinda tena.”

Kujiondoa kwa Rais Biden kutoka kwenye ushindani jana Jumapili, kama Harris atateuliwa, kwa mara nyingine tena ataweka historia kama mwanamke wa kwanza mweusi na Mmarekani mwenye Asilia ya India kuwania nafasi ya juu kabisa katika nchi.

Kamala Harris, Makamu Rais, Marekani alihitimisha kwa kusema: “Mungu awabariki na Mungu aibariki Marekani.”

Forum

XS
SM
MD
LG