Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 16, 2024 Local time: 22:05

Sitisha mapigano sasa hivi, Makamu Rais Harris awaambia Israeli na Hamas


Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris. Machi 3, 2024.
Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris. Machi 3, 2024.

Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris Jumapili alitoa wito wa sitisho la mara moja la mapigano katika ukanda wa Gaza na kuishinikiza kwa dhati Israel kuongeza usambazaji wa misaada ili kupunguza kile alichokiita “hali isiyo ya kibinadamu” na “janga la kibinadamu” miongoni mwa Wapalestina.

Harris, ambaye alikuwa akizungumza kwenye hafla huko Selma jimbo la Alabama, kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji mabaya au “Bloody Sunday”, ambapo wanajeshi wa jimbo hilo waliwapiga watu waliokuwa wakiandamana kwa amani, aliihimiza Hamas kukubali makubaliano ya kuwaachia huru mateka ambayo yatakuwa mwanzo wa sitisho la mapigano kwa kipindi cha wiki sita na kuruhusu usambazaji wa misaada kwa wingi.

“Watu wa Gaza wanakabiliwa na njaa. Hali ni ya kinyama na ubinadamu wetu wa pamoja unatulazimisha kuchukua hatua,” Harris alisema.

“Serikali ya Israel lazima ifanye juhudi zaidi kwa kuongeza vya kutosha usambazaji wa misaada kwa wingi. Hakuna visingizio hapa.”

Israel ilisusia mazungumzo ya kusitisha mapigano huko Gaza mjini Cairo Jana Jumapili baada ya Hamas kutupilia mbali ombi la Israel la kuwaachilia mateka wote ambao bado wako hai, kulingana na gazeti moja la Israel.

“Hamas inadai inataka sitisho la mapigano. Sawa, kuna makubaliano mezani. Na kama tulivyosema, Hamas lazima iridhie makubaliano hayo,” Harris alisema. “Acha tupate makubaliano. Acha tuunganishe mateka na familia zao. Na acha tutoe afueni kwa watu wa Gaza,” aliongeza.

Forum

XS
SM
MD
LG