Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:31

Meli ya mizigo liyoshambuliwa kwenye bahari ya Shamu yazama


Picha ya maktaba ya meli ya mizigo kwenye bahari ya Shamu.
Picha ya maktaba ya meli ya mizigo kwenye bahari ya Shamu.

Maafisa wa kulinda bahari wamesema Jumamosi kwamba meli ilioshambuliwa na waasi wa-Houthi wa Yemen, imezama siku kadhaa baada ya tukio hilo, ikiwa ya kwanza kuharibiwa kabisa tangu kampeni  ya mashambulizi ilopoanza kwenye bahari ya Shamu.

Operesheni ni kama njia ya kushinikiza Israel kusitisha mashambulizi yake dhidi ya Hamas kwenye Ukanda wa Gaza. Kuzama kwa meli hiyo kwa jina Rubymar iliyokuwa na bendera ya Belize, kumetokea wakati meli za mizigo kutoka Asia na Ulaya zikiendelea kuathiriwa na mashambulizi ya wa-Houthi, baadhi zikilazimika kutafuta njia mbadala.

Kuzama kwa meli hiyo huenda kukaongeza idadi ya meli zinazotafuta njia mbadala na kupelekea kuongezwa kwa bima, kuongezeka kwa bei za bidhaa, pamoja na kuathiriwa kwa shuguli za uchukuzi wa meli wa kieneo kwa ujumla. Serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa, pamoja na afisa wa kundi la kijeshi lililopo huko wamedhibitisha kuwa meli hiyo ilizama.

Afisa huyo alizungumza bila kujitambulisha kwa kuwa hakuwa na idhini yoyote ya kuongea na vyombo vya habari. Meneja wa meli hiyo mwenye makao yake Beirut hakupatikana ili kutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo. Serikali ya Yemen iliopo uhamishoni , na inayoungwa mkono na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia tangu 2015, imesema kwamba Rubymar, ilizama Ijumaa jioni kufutia mawimbi makubwa kweye bahari ya Shamu.

Forum

XS
SM
MD
LG