Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:37

Viongozi wakutana Munich kujadili usalama na vita


Wanasiasa wa ngazi ya juu, maafisa wa kijeshi na wanadiplomasia kutoka kote ulimwenguni wamekusanyika mjini Munich, Ujerumani Ijumaa kwa mkutano wa usalama utakaotawaliwa na vita vya Israel na Ukraine pamoja na hofu juu ya ahadi ya Marekani ya kutetea washirika wake.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, makamu wa rais wa Marekani, Kamala Harris, na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, ni miongoni mwa viongozi na maafisa wanaohudhuria mkutano wa usalama wa Munich (MSC), ambao ni mkutano wa kila mwaka wa kimataifa ukilenga ulinzi na diplomasia.

Rais wa Israel Isaac Herzog, na Waziri Mkuu wa Palestina, Mohammad Shtayyeh, pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano ulioanza leo na kwenda mpaka Jumapili katika hoteli mji wa kusini mwa Ujerumani.

Mkutano huo unafanyika huku vita vya Gaza vikiingia mwezi wa tano ambapo Wapalestina 28,000 na Waisraeli 1,430 wameuwawa.

Forum

XS
SM
MD
LG