Vivian Cheruiyot alishinda medali mbili katika michezo ya Olimpiki Rio 2016 - dhahabu katika mita 5000 na shaba katika mita 10000
Mtanzania Alphonse Felix Simbu ashika nafasi ya tano na Mganda Solomon Mutai ashika nafasi ya nane katika mbio hizo za Rio de Janeiro
Kutoka Rio 2016 Idd Ligongo anakuletea kinachoendelea sasa.
Kenya sasa inaongoza bara la Afrika kwa kuwa na jumla ya medali nane, nne za dhahabu, tatu za fedha na moja ya shaba. Afrika Kusini inashika nafasi ya pili kwa jumla ya medali sita
Kenya sasa yaongoza Afrika kwa kuwa na medali tatu za dhahabu na tatu za fedha, ikifuatiwa na Afrika Kusini ambayo ina dhahabu moja, fedha nne na shaba moja
Hii ni medali ya pili ya dhahabu kwa Kenya katika michezo ya Olimpiki inayoendelea huko Rio de Janeiro baada ya Jemima Sumgong kushinda medali ya dhahabu katika fainali ya mbio ndefu - marathon
Wabrazil wa vitongoji vya watu maskini walalamika kutokana na maisha magumu wanaokabiliana nao licha ya kufanikiwa kwa michezo ya Olimpik
Mjamaica Usain Bolt ndiye mtu wa kwanza kushinda dhahabu mara tatu mfululizo katika mbiyo za mita 100 kwenye michezo ya Olimpiki.
Sumsong mwenye umri wa miaka 31 alimaliza mbio hizo kwa saa mbili, dakika 24 na sekunde nne, na kumshinda Eunice Kirwa wa Bahrain na Mare Dibaba wa Ethiopia.
Vivian Cheruiyot wa Kenya alishika nafasi ya pili na kupata medali ya fedha ikiwa medali ya kwanza kwa Kenya katika michezo ya Olimpiki ya Rio 2016
Anzrah ni afisa wa pili wa timu ya Kenya kuingia mashakani katika muda wa wiki moja. Maafisa wa Olimiki wamesema kuwa alijitambulisha kama Cheruiyot Ferguson Rotich mwanariadha anyeshiriki kwa mashindano ya Rio.
Pandisha zaidi