Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 22:55

Bolt ashinda 100m katika Olimpiki mara ya tatu


Usain Bolt de la Jamaïque court à côté de James Dasaolu de la Grande-Bretagne lors de 100 mètres-messieurs aux Jeux Olympiques d'été de 2016 au stade olympique à Rio de Janeiro, au Brésil, 13 août 2016.
Usain Bolt de la Jamaïque court à côté de James Dasaolu de la Grande-Bretagne lors de 100 mètres-messieurs aux Jeux Olympiques d'été de 2016 au stade olympique à Rio de Janeiro, au Brésil, 13 août 2016.

Mkimbiaji wa kazi kuliko wote duniani, Usain Bolt, aliweka historia Jumapili aliposhinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 na kumfanya mtu wa kwanza kushinda dhahabu mara tatu mfululizo katika mbio hizo kwenye michezo ya Olimpiki.

Bolt, Raia wa Jamaica, alipata ushindi huo wa kipekee alipokimbia akitumia muda wa sekunde 9.58, na kukaribia mno kuivunja rekodi ya dunia.

Alifuatiwa na Mmarekani Justin Gatlin aliyechukua medali ya fedha huku nambari ya tatu ikitwaliwa na Adress de Gresse wa kutoka Canada.

Umati mkubwa uliokusanyika katika uwanja mmoja nchini Jamaica ulishangilia kwa shangwe na vigelegele punde tu Bolt alipomaliza mbio hizo.

Mapema Jumapili, Jemimah Jeptoo Sumgong aliipatia Kenya medali ya kwanza ya dhahabu baada ya kushinda mbio za marathon kwenye mashindano hayo. Hiyo pia ilikuwa medali ya kwanza ya Kenya katika marathon ya wanawake katika michezo ya Olimpiki.

Sumsong mwenye umri wa miaka 31, alimaliza mbio hizo kwa saa mbili, dakika 24 na sekunde nne, na kumshinda Eunice Kirwa wa Bahrain aliyechukua medali ya fedha. Nafasi ya tatu ilimwendea Muethiopia Mare Dibaba.

Katika mbio za mita mia nne zilizofanyika siku ya Jumapili pia, Wade Van Niekerk wa Afrika kusini, alipata dhahabu, huku akiweka rekodi mpya ya dunia.

XS
SM
MD
LG