Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 04:16

Sumgong aipatia Kenya dhahabu ya kwanza Rio


Jemima Sumgong (KEN) of Kenya celebrates after winning the Women's Marathon, Aug. 14, 2016.
Jemima Sumgong (KEN) of Kenya celebrates after winning the Women's Marathon, Aug. 14, 2016.

Jemimah Jeptoo Sumgong aliipatia Kenya medali ya kwanza ya dhahabu Jumapili baada ya kushinda mbio za marathon kwenye mashindano ya Olimpiki mjini Rio De Jenairo, Brazil.

Hii pia ni medali ya kwanza ya Kenya katika marathon ya wanawake katika michezo ya Olimpiki

Sumsong mwenye umri wa miaka 31, alimaliza mbio hizo kwa saa mbili, dakika 24 na sekunde nne, na kumshinda Eunice Kirwa wa Bahrain aliyechukua medali ya fedha. Nafasi ya tatu ilimwendea Muethiopia Mare Dibaba.

“Sikuwa na shaka kwamba ningeshinda mbio hizi,” Sumgong aliwwambia waandishi wa habari muda mfupi baada ya ushindi huo.

Ushindi wake uliipatia Kenya medali ya tatu katika mashindano hayo ya msimu wa kiangazi.

Mwanariadha huyo alipata umaarufu mwezi Aprili mwaka huu baada ya kushinda dhahabu katika mashindano ya mbio za Marathon za London, licha ya kujikwaa na kuanguaka kabla ya mbio hizo kumalizika.

Medali yake ilifuata ile ya mwenzake, Vivian Jepkemoi Cheruiyot, aliyechukua nafasi ya pili siku ya Jumamosi, na hivyo basi kupata fedha baada ya kukimbia kwa muda wa dakika 29 na sekunde 32.53.

Cheruiyot ambaye ni mshindani wa siku nyingi wa wanariadha wa Ethiopia alijikuta ametokwa ghafla na Ayana, lakini alijitahidi kushikilia nafasi ya pili na kumwacha Dibaba akishika nafasi ya tatu.

Wakenya wengine wawili walishika nafasi za nne na tano. Alice Aprot Nawowuna akimaliza katika muda wa dakika 29:53.51 akifuatiwa na Betsy Saina aliyemaliza katika muda wa dakika 30:07.78.

Diane Nukuri wa Burundi alimaliza katika nafasi ya 13 katika muda wa dakika 31:28.69, na Salome Nyirarukundo wa Rwanda alimaliza katika nafasi ya 27 katika muda wa dakika 32:07.80.

Cheruiyot amekuwa mwanariadha wa kwanza wa Kenya kuipatia nchi yake medali katika michezo ya Olimpiki ya Rio 2016.

XS
SM
MD
LG