Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 17:35

Kocha wa Kenya afukuzwa Rio kwa 'udanganyifu'


Ferguson Cheruiyot Rotich akiongoza kundi la wanariadha katika mbio za mita 800 Bejing
Ferguson Cheruiyot Rotich akiongoza kundi la wanariadha katika mbio za mita 800 Bejing

John Anzrah , kocha wa mbiyo fupi wa timu ya wanariadha wa Kenya amerudishwa nyumbani kutoka michezo ya Olympiki inayoendelea huko Rio baada ya kujitambulisha kua ni mwanariadha na hata kutoa mkojo ili kupimwa.

Kufuatana na mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Olympik ya Kenya Kipchoge Keino, kocha Anzrah alijitambulisha kama Ferguson Rotich anaetarajiwa kuwika katika mbio za mita 800 wakati alipoulizwa na maafisa wa Olimpik kuhusu kupimwa mkojo wake.

Kieno anasema "hatuwezi kustahamili tabia kama hiyo na hata hawafahamu jinsi alivyowasili huko, kwani kamati yetu haikushughulikia safari yake."

Tukio hilo ni la pili katika kipindi cha wiki moja ambapo afisa wa riadha ya Kenya anarudishwa nyumbani kutoka Rio kuhusiana na masuala ya utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu na ni dosari katika lile suala la ikiwa Kenya kweli inachukua hatua zinazostahiki kupambana na tatizo hilo.

Wiki iliyopita meneja wa timu ya riadha Michael Rotich, alikrudishwa nyumbani baada ya kusema aliomba fedha ili kutoa habari juu ya lini wataalmu wa kupima dawa za kuomgeza nguvu watakapowasili.

Kabla ya mashindano ya mwaka huu kuanza mjini Rio, wasiwasi ulikuwa umetanda kuhusu kushiriki kwa timu ya Kenya baada ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kudai kuwa baadhi ya wanariadha wa Kenya hawakufanyiwa vipimo hivyo ipasavyo.

Hata hivyo, shirika linaloshughulikia madai ya matumizi dawa za kusisimua misuli (WADA), liliiondolea lawama timu ya Kenya na kuitoa kwenye orodha hiyo siku ya Ijumaa wiki wiki iliyopita, saa chache tu kabla ya michezo hiyo ya Olimpiki kufunguliwa rasmi.

Zaidi ya wanariadha 40 kutoka Kenya wamepigwa marufuku kushiriki riadha tangu mwaka wa 2011 baada ya kupatikana wametumia dawa za kuongeza nguvu misuli.

XS
SM
MD
LG