Angalia ziara ya Papa Francis Afrika. Akitembelea Kenya, Uganda, na Central African Republic.
Papa Francis ametoa wito wa Umoja huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuwataka wananchi kutoruhusu tofauti za kidini kuwagawanya, akiwa katika kituo cha mwisho cha ziara yake ya Afrika.
Papa Francis awataka Waganda kuwasaiudia wenzao katika kumtumikia Mungu
Papa Francis aliwahimza waganda kuwatumikia wenzao kwa moyo wa ubinadamu na unyeyekevu, hasa wazee, maskini na waloachwa au kupoteza familia zao,
Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya Uganda Pape Francis ameongoza misa yake ya kwanza nchini humo, na kuzungumza na vijana, akisena dunia inaiangalia Afrika kama bara la matumaini.
Papa Francis amewalaumu matajiri wanaohusika na rushwa na kutaka juhudi zifanyike kupambana na tatizo kubwa la ukabila nchini Kenya.
Papa Francis Awasili Uganda kuendelea na ziara yake ya Afrika
Papa Francis ameongoza misa yake ya kwanza Afrika mjini Nairobi kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi akitoa wito kwa upendo amani na muelewano.
Maelfu ya waumini wa kanisa katoliki wakiandamana na watu wa tabaka mbalimbali walikusanyika katika uwanja wa chuo kikuu cha Nairobi huko nchini Kenya siku ya Alhamisi hili kumuona na kumsikiliza kiongozi wa Kanisa la Katoliki duniani, Papa Francis, akiongoza misa yake ya kwanza barani Afrika.
Tunamatumaini kwamba ziara ya papa itaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa mioyo ya watu wa jamhuri ya afrika ya kati, ambayo itapelekea kurejea Amani na kurejea kwa waislamu na wakristo kuishi pamoja. Hili litapelekea maendeleo ya taifa.
Pandisha zaidi