Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 23:34

Maelfu wahudhuria ibada ya Papa Nairobi


Watu wamsubiri Papa Francis katika uwanja wa chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya siku ya Alhamisi Nov. 26, 2015.
Watu wamsubiri Papa Francis katika uwanja wa chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya siku ya Alhamisi Nov. 26, 2015.

Maelfu ya waumini wa kanisa la katoliki wakiandamana na watu wa tabaka mbalimbali walikusanyika katika uwanja wa chuo kikuu cha Nairobi huko nchini Kenya siku ya Alhamisi hili kumuona na kumsikiliza kiongozi wa Kanisa la Katoliki duniani, Papa Francis, akiongoza misa yake ya kwanza barani Afrika.

Huku wakistahimili mvua kubwa na baridi kali, watu hao walimsikiliza kwa makini kiongozi huyo wa Vatican akiongoza maombi kwa lugha ya kilatini, ambayo yalitafsiriwa kwa lugha ya kingereza.

Papa Francis alisisitiza umuhimu wa Amani na kusema kwamba watu hawafai kuzozana au hata kuuana kwa sababu ya tofauti za kidini.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:20 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kulikuwa na ulinzi mkali katika bustani ya chuo hicho, ambapo zaidi ya mafisa elfu 15 wa usalama walilinda doria.

Barabara muhimu zimefungwa, hali ambayo ilisababisha tatizo kubwa la usafiri mjini Nairobi.

Kulingana na ratiba rasmi, kabla ya kuondoka hapa Nairobi Papa Francis alipangiwa kuhutubia vijana katika uwanja wa michezo ya kasarani na vilevile kutembelea makao makuu ya shirika la mazingira la umoja wa mataifa.

Kadhalika alitarajiwa kuongoza misa takatifu katika mtaa ya watu maskini wa kangemi.

Baada ya kukamilisha ziara yake nchini Kenya, Papa Francis atazuru nchi ya Uganda na Central Africa Republic yaani Jamhuri ya Afrika ya kati.

XS
SM
MD
LG