Uchunguzi na msako unaendelea katika wilaya ya Kasese magharibi ya Uganda kufuatia ghasia kati ya polisi na vijana na kusababisha vifo vya watu 7 na wengine kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wetu Kennes Bwire, aliyeko Kampala, Uganda, vitu vilivyoibiwa ni pamoja na tarakilishi na karatasi zinazoelezwa kuwa na ushahidi muhimu.
Mawakili wa Amama Mbabazi walifanyia mabadiliko ya orodha ya mambo mahakama hiyo inafaa kushughulikia.
Chama kikuu cha upinzani nchini Uganda cha Forum for Democratic Change, FDC kimezuiliwa kuwasilisha malalamishi yake mahakamani kuhusu matokeo ya uchaguzi uliomalizika.
Mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani walimtembelea kiongozi wa upinzani wa Uganda Kizza Besigye, siku ya Ijumaa na kumsihi kutotumia lugha itakayo chochea mvutano na ghasia nchini humo
Tume ya uchaguzi kwa mara ya kwanza katika historia ya Uganda ilitangaza matokeo rasmi ya kiti cha Meya katika jimbo la Kampala majira ya saa kumi na moja alfajiri siku ya Alhamis.
Upinzani nchini Uganda umesema hauwezi kuacha haki yao ipotee na kwamba watafuata sheria zote za nchi kudai haki yao baada ya uchaguzi wa Februari 18
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu nchini Uganda yameeleza kughadhabishwa na jinsi polisi wanavyomkamata kinara wa chama cha Forum for democratic change âFDC â Dkt Kiiza Besigye yakisema haikubaliki kisheria.
Besigye alionekana mtulivu na hakusema lolote wakati alipokuwa anavutwa na kuingizwa kwenye gari la polisi.
Rais mteule wa Uganda, Yoweri Museveni amesema hakuna yeyote anayeweza kumshauri kuhusu uongozi wa nchi yake.
Usalama umeimarishwa Kampala wakti Museveni anakanusha kulikuwepo na wizi ulopangwa na hatoruhusu ghasia kuzuka nchini mwake, huku kiongozi wa upinzani Besigye akisema wananchi watatetea haki zao kwa kukaidi amri za utawala.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani imepongeza watu wa Uganda bila kutamka waziwazi kuwa inampongeza Rais Museveni katika ushindi wake. Museveni alitangazwa mshindi kuendelea na utawala kwa miaka mingine mitano
Pandisha zaidi