Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 08:29

Marekani yapongeza watu wa Uganda


Mark Toner, msemaji wa Marekani
Mark Toner, msemaji wa Marekani

Marekani imewapongeza watu wa Uganda kwa kushiriki kikamilifu na kwa amani katika uchaguzi wa Uganda Februari 18.

Katika tamko lililotolewa na msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Mark Toner, Marekani imesema ingawa hakukua na machafuko makubwa, ni budi kutilia maanani kuwa ripoti nyingi za hitilafu na utendaji mbaya wa maafisa kunaleta wasiwasi na ni kinyume na viwango vya kimataifa na matazamio ya utaratibu wa kidemokrasia.

Ucheleweshaji wa vifaa vya kupigia kura, ripoti za makaratasi ya kura zilizopigwa kabla, ununuaji wa kura na kuzuiliwa kwa mitandao ya kijamii pamoja matumizi ya nguvu yaliyofanywa na polisi kwa pamoja kunadhalilisha utaratibu wa uchaguzi.

Taarifa hiyo imesema kuwa Marekani pia "in a wasiwasi kuhusu kuendelea kuwekwa katika kizuizi cha nyumbani mgombea wa upinzani Kizza Besiege. Marekani "inatoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa (Besigye) na kufunguliwa kwa mitandao ya kijamii."

XS
SM
MD
LG