Chama kikuu cha upinzani nchini Uganda cha Forum for Democratic Change, FDC, kinataka tume huru ya wakaguzi kuundwa ili kufanya uchunguzi wa kina wa jinsi uchaguzi mkuu ulivyofanyika nchini humo.
Haya yanajiri baada ya polisi kuwazuilia wakuu wa chama hicho pamoja na Dkt Kiiza Besigye aliekuwa mgombea wake wa urais, kufika mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita na ambao ulimpa Rais Yoweri Museveni ushindi.