Mkuu wa polisi wa Uganda Jenerali Edward Kale Kayihura, anesema ghasia zilizosababisha vifo vya watu 7 katika wilaya ya Kasese, magharibi ya nchi huwenda zimechochewa na wakuu wa kifalme wa eneo hilo.
Akizungumza na waandishi habari Jumapili baada ya kutembelea eneo la ghasia anasema, watu watatu walokamatwa wanauhusiano na ufalme wa kijadi wa Ruwenzuri.
Watu hao waliuwawa baada ya kutokea mapambano kati ya polisi na vijana walokua wanataka kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa serikali ya mitaa.
Polisi walokua na bunduki walifyetua kwanza risasi hewani kujaribu kuwatawanya vijana lakini baada ya kukataa mapmabano yalianza kati ya polisi na vijana walokua na vijiti. Polisi waliwafyetulia vijana hao risasi na kuwauwa waandamanaji sita papo hapo.
Mkuu wa polisi anasema uchunguzi unaendelea na watu zaidi huwenda wakakamatwa kutokana na tukio hilo.