Rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni, amesema hakuna mtu anaeweza kumshauri jinsi ya kuongoza Serikali yake, akisema ripoti ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya inayosema uchaguzi mkuu uliomrudisha madarakani ulikumbwa na dosari chungu nzima, ni upuzi mtupupu.
Museveni pia ameonya kwamba Serikali yake sio kitu cha kuchezea na kwamba anaweza kufanya makubwa, huku Kiongozi wa chama cha FDC Dkt Kiiza Besigye, anayedai kuibiwa kura akisema atatoka nyumbani kwake kwa lazima leo Jumatatu baada ya kuzuiliwa na maafisa wa usalama akisema kuwa kwake nyumbani sio Jela.