Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu nchini Uganda yameeleza kughadhabishwa na jinsi polisi wanavyomkamata kinara wa chama cha Forum for democratic change –FDC – Dkt Kiiza Besigye yakisema haikubaliki kisheria.
Hii inafuatia hatua ya polisi kumwachilia Besigye siku ya Jumatatu na tena kurauka nyumbani kwake siku ya Junmanne, kumkamata na kumpeleka sehemu ambayo haikuwa imejulikana kufikia wakati wetu kwenda mitamboni. Besigye amepinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika wiki jana ambapo rais wa sasa Yoweri Museveni alitangazwa mshindi.
Mwandishi wetu wa Kampala Kennes Bwire anaripoti.