Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 07:34

Zaidi ya watu 61,000 wafariki kutokana na vita Sudan


Kifaru cha jeshi kikionekana mtaani kikiwa kimeharibika huko Omdurman, Sudan Aprili 7, 2024. Picha na REUTERS/El Tayeb Siddig
Kifaru cha jeshi kikionekana mtaani kikiwa kimeharibika huko Omdurman, Sudan Aprili 7, 2024. Picha na REUTERS/El Tayeb Siddig

Zaidi ya watu 61,000 wanakadiriwa kufariki dunia huko Khartoum katika kipindi cha miezi 14 ya vita vya Sudan.

Huku ushahidi ukionyesha kuwa kutokana na mzozo huu mbaya huenda idadi ikawa kubwa zaidi kuliko ilivyorekodiwa awali, kwa mujibu wa ripoti ya watafiti kutoka Uingereza na Sudan.

Idadi hiyo inajumuisha watu takriban 26,000 waliouwawa kikatili, idadi inakadiriwa ni kubwa zaidi ya ile inayotumiwa hivi sasa na Umoja wa Mataifa kwa nchi nzima.

Utafiti wa awali uliofanywa na kundi la utafiti kutoka London school of hygiene na kundi la utafiti wa madawa ya tropiki sudan umependekeza kwamba njaa na magonjwa vinazidi kuwa sababu kuu za vifo kote Sudan.

Makadirio ya vifo kutokana na sababu zote mjini Khartoum vilikuwa katika kiwango cha asilimia 50 juu zaidi kuliko wastani wa kitaifa kabla ya ghasia zilizosababishwa na jeshi la taifa na kundi la Rapid Support Forces Aprili mwaka 2023, watafiti wamesema.

Umoja wa mataifa umesema mzozo huo umewakosesha makazi zaidi ya watu milioni 11 kutoka kwenye nyumba zao na kupelekea mzozo mkubwa wa njaa duniani . Zaidi ya watu milioni 25 nusu ya idadi ya watu wa Sudan wanahitaji msaada wakati njaa imeikumba kambi moja ya wasiokuwa na makazi.

Forum

XS
SM
MD
LG