Rasimu hiyo inazitaka pande zinazopigana nchini Sudan zisitishe uhasama na kuzitaka kuruhusu upelekaji salama wa misaada, wa haraka na bila vikwazo kote kwenye mstari wa mbele na mipakani.
Mgogoro wa Sudan ulianza Aprili 2023 kutokana na mapambano ya madaraka kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka vya kijeshi kabla ya mpango wa mpito kuelekea utawala wa kiraia, na kusababisha mgogoro mkubwa sana wa ukosefu wa makazi.
Vita hivyo vimezalisha mawimbi ya ghasia yanayochochewa kikabila ambapo kundi la RSF linalaumiwa.
Rasimu hiyo inatoa wito kwa kivuko cha mpaka cha Adre na Chad kubaki wazi kwa ajili ya kuwasilisha misaada kupitia vivuko vyote vya mpaka, wakati mahitaji ya kibinadamu yanaendelea, na bila vikwazo.
Uingereza ililenga rasimu ya azimio ipigiwe kura haraka iwezekanavyo, kwa mujibu wanadiplomasia hata hivyo Ili kupitishwa, azimio linahitaji angalau kura tisa za kuunga mkono na hakuna kura ya turufu kutoka kwa Marekani, Ufaransa, Uingereza, Russia au China.
Forum