Waziri mkuu wa Haiti Garry Conille alianza ziara huko Umoja wa Falme za Kiarabu na Kenya mwishoni mwa juma kutafuta msaada wa usalama, baada ya moja ya mashambulizi mabaya ya magenge ambayo nchi hiyo haijawahi kushuhudia katika miaka ya hivi karibuni.
Mwenyekiti wa kampuni ya mafuta ya Total Energies, Patrick Pouyanne ambaye pia ni mkurugenzi mkuu amesema Jumatano kwamba anapanga kuzuru Msumbiji baadaye mwezi huu kwa ajili ya mpango wa kuwekeza nchini humo.
Washika dau wakuu kwenye Shirika la Kimataifa la Fedha, IMF, wamesihi Kenya itoe ombi kwa IMF la kuchunguza madai ya ufisadi na utalawa mbaya, kama hatua kuelekea kupata mikopo iliyokwama kufuatia kusitishwa kwa mswada wa fedha uliolenga kuongeza kodi.
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris Alhamisi aliahidi msaada kwa Ukraine, akimuzungumzia mpinzani wake Donald Trump bila kumtaja jina, akisema wale ambao wanataka Ukraine ibadilishe ardhi yake kwa ajili ya amani na Russia, wanaunga mkono “mapendekezo ya kujisalimisha.”
Jeshi la Sudan limefanya mashambulizi ya mizinga na ya anga katika mji mkuu wa Sudan Alhamisi katika operesheni kubwa sana ya kukomboa tena maeneo ya huko tangu vita vyake vya miezi 17 kuzuka na vikosi vya RSF , mashahidi na vyanzo vya jeshi vimesema.
Ibada ya kumbukumbu imefanyika leo Alhamisi kwa ajili ya wavulana 21 waliofariki katika ajali ya moto kwenye shule mapema mwezi huu.
Benki ya dunia Jumatatu ilisema kwamba Denmark imeahidi kutoa mchango wa dola milioni 491.7 kwa mfuko wa benki hiyo ili kusaidia nchi maskini, likiwa ongezeko la asilimia 40 ikilinganishwa na mchango wa awali wa nchi hiyo.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema hatawania muhula wa nne mfululizo wa urais ikiwa atashindwa kwenye uchaguzi wa tarehe 5 Novemba, akisema hayo katika mahojiano yaliyochapishwa Jumapili.
Kikosi cha mapinduzi cha Iran Jumapili kilisema kiliwakamata watu 12 kwa kuwa majasusi wanaoshirikiana na Israel ambao walikuwa wanapanga vitendo vya kuvuruga usalama wa Iran.
Ofisi ya rais wa Nigeria imesema Alhamisi kwamba kampuni ya Coca Cola inapanga kuwekeza dola bilioni moja kwenye operesheni zake nchini humo ndani ya miaka mitano ijayo kufuatia mkutano kati ya wakurugenzi wake na Rais Bola Tinubu.
Mamlaka za Nigeria zimesema Jumatatu kuwa wafungwa 281 wametoroka baada ya mafuriko kuangusha kuta za jela kaskazini mashariki mwa nchi.
Kenya imetoa kadarasi ya usambazaji wa umeme kupitia ushirikiano na sekta ya kibinafsi na kampuni ya Adani ya India, pamoja na benki ya Maendeleo ya Afrika, kulingana na mshauri mkuu wa kiuchumi wa rais, David Ndii.
Ukraine Alhamisi iliishtumu Russia kwa kutumia makombora ya kimkakati kushambulia meli ya nafaka ya kiraia katika shambulizi la kombora katika bahari ya Black Sea karibu na Romania, nchi mwanachama wa NATO, na kuzidisha mvutano kati ya Moscow na muungano huo wa ushirika wa kijeshi.
Marekani inaunga mkono hatua ya kuongeza viti viwili vya kudumu kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa ajili ya mataifa ya Afrika.
Kundi la wanamgambo la Hamas Jumatano lilisema kwamba wapatanishi wake wamesisitiza utayari wake wa kutekeleza sitisho la vita la “mara moja” na Israel huko Gaza, kulingana na pendekezo la hapo awali la Marekani bila masharti ya kutoka upande wowote.
Mahakama ya Juu ya Kenya imesitisha kwa muda mkataba wa kukodishwa kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta – JKIA, kwa muda wa miaka 30, kwa kampuni ya India ya Andani Group, kwa lengo la kuupanua.
Aliyekuwa mpenzi wa mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei, anayedaiwa kumuuwa kwa kumchoma baada ya kummwagia petroli, ameripotiwa kufariki pia, kutokana na majeraha ya moto aliyopata wakati wa tukio hilo.
Rais wa Algeria Abdulmadjid Tebboune ameshinda uchaguzi wa urais nchini Algeria na ushindi wake kuangaziwa zaidi na vyombo vya habari nchini humo.
Mgombea wa upinzani kwenye uchaguzi wa rais nchini Venezuela Edmundo Gonzalez alisafiri kuelekea Uhispania kuomba hifadhi, Madrid imesema.
China Jumapili ilisema itaruhusu kuanzishwa kwa hospitali zinazomilikiwa na wageni katika maeneo tisa ya nchi ikiwemo mji mkuu, huku Beijing ikijaribu kuvutia zaidi uwekezaji wa kigeni ili kukuza uchumi wake unaosusua.
Pandisha zaidi