Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 07:53

Wasiwasi waongezeka wakati Netanyahu akitishia kufanya mashambulizi zaidi Beirut


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Wakaazi wa mji mkuu wa Lebanon Beirut Jumanne wameendelea kuwa na wasiwasi baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kutishia kuendelea na mashambulizi dhidi ya Hezbollah kote Lebanon pamoja na mji mkuu.

Netanyahu alitembelea kambi ya jeshi katikati mwa Israel ambako wanajeshi wanne waliuwawa Jumapili na ndege zisizokuwa na rubani za Hezbollah, alisema Jumatatu Israel iliendelea kulishambulia kundi hilo linaloungwa mkono na Iran, bila kuwa na huruma kote Lebanon ikiwemo Beirut.

Shambulizi la angani lililofanywa na jeshi la Isreali Jumatatu katika kijiji cha Aito, kaskazini mwa Lebanon. Picha imetolewa Jumanne Oktoba 15, 2024. (AP Photo/Hussein Malla)
Shambulizi la angani lililofanywa na jeshi la Isreali Jumatatu katika kijiji cha Aito, kaskazini mwa Lebanon. Picha imetolewa Jumanne Oktoba 15, 2024. (AP Photo/Hussein Malla)

Jumanne wakaazi wa Beirut walionekana wakiendelea na shughuli zao za kawaida, wakinywa kahawa, mikate na kuvuta shisha.

Mzozo kati ya Israel na Hezbollah ulianza mwaka mmoja uliopita wakati kundi hilo la wanamgambo lilipofyatua roketi Israel kwa lengo la kuliunga mkono kundi la wanamgambo la Hamas wakati wa kuanza vita vya Gaza.

Jeshi la Israeli limesema kuwa operesheni zake zina lengo la kuhakikisha kurejea maelfu ya watu waliokoseshwa makazi kaskazini mwa Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG