Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 22:47

Watoto 400,000 wakoseshwa makazi Lebanon kutokana na mapigano-UNICEF yasema


Watoto waliochukua hifadhi kwenye shule mjini Beirut, Lebanon. Oktoba 3, 2024.
Watoto waliochukua hifadhi kwenye shule mjini Beirut, Lebanon. Oktoba 3, 2024.

Afisa mmoja wa ngazi wa juu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia watoto, UNICEF, amesema Jumatatu kwamba zaidi wa watoto 400,000 wa Lebanon wamekoseshwa makazi ndani ya wiki tatu zilizopita.

Afisa huyo ameonya kuhusu kuwepo kwa kizazi kilichopotea kwenye taifa hilo ndogo linalokabiliwa na majanga kadhaa ikiwemo vita vinavyoendelea. Israel imeongeza kampeni ya mashambulizi dhidi ya kundi la wanamgambo la Hezbollah la Lebanon, yakiwemo mashambulizi ya ardhi, baada ya mwaka mmoja wa makabiliano na kundi la Hamas huko Gaza.

Mapigano ya Lebanon yamelazimisha takriban watu milioni 1.2 kutoroka makwao wengi wakitorokea Beirut pamoja na maeneo mengine ya kaskazini katika wiki 3 zilizopita. Ted Chaiban ambaye ni naibu mkurugenzi wa masuala ya kibinadamu kwenye UNICEF, alitembelea baadhi ya shule ambazo zimegeuzwa kuwa hifadhi ya familia zilizokoseshwa makazi.

Chaiban aliambia shirika la habari la AP, kwamba kilichomshangaza ni idadi kubwa ya watoto walioathiriwa licha ya kuwa vita hivyo vimechukua wiki tatu pekee.

Forum

XS
SM
MD
LG