Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 11:00

Waziri mkuu wa Haiti atembelea UAE na Kenya baada ya magenge kuua watu 70


Waziri mkuu wa Haiti Garry Conille.
Waziri mkuu wa Haiti Garry Conille.

Waziri mkuu wa Haiti Garry Conille alianza ziara huko Umoja wa Falme za Kiarabu na Kenya mwishoni mwa juma kutafuta msaada wa usalama, baada ya moja ya mashambulizi mabaya ya magenge ambayo nchi hiyo haijawahi kushuhudia katika miaka ya hivi karibuni.

Wanamgambo wa kundi la magenge la Gran Grif walishambulia mji wa magharibi mwa Artibonite wa Pont-Sonde siku ya Alhamisi, na kuua watu 70, wakiwemo watoto, na kulazimisha zaidi ya wakazi 6,000 kukimbia.

Kabla ya ziara hiyo, Conille aliwatembelea waathirika wa shambulizi hilo kwenye hospitali ya karibu, ambako alisema serikai yake itatenga rasilimali za kuimarisha usalama huko Pont-Sonde.

Mauaji hayo yalisababisha mshutuko mkubwa katika nchi ambayo imezoea kuibuka kwa ghasia na kuwepo kwa idadi ndogo ya polisi.

“Magenge yanadhibiti eneo hilo, yameliharibu,” amesema mkazi wa eneo hilo Roseline.

“Wamefyatulia risasi watu wengi, imetuathiri sana.”

Akiwa huko Umoja wa Falme za Kiarabu, Conille alisema atajadili na mwenzake jinsi ya kupeleka idadi kubwa ya polisi kusaidia polisi wa Haiti kurejesha usalama.

Baadaye ataondoka UAE kuelekea Nairobi, Kenya.

Forum

XS
SM
MD
LG