Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 17, 2024 Local time: 08:38

Biden na Netanyahu wajadili mpango wa Israel kuishambulia Iran


Rais Joe Biden akikutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika ofisi ya rais ya White House, Julai 25. 2024. Picha ya AP
Rais Joe Biden akikutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika ofisi ya rais ya White House, Julai 25. 2024. Picha ya AP

Rais wa Marekani Joe Biden na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walizungumza Jumatano kuhusu mpango wa Israel wa kulipiza kisasi dhidi ya Iran, huku kundi la Hezbollah likisema wapiganaji wake waliwarudisha nyuma wanajeshi wa Israel kwenye eneo la mpakani.

Mapigano ya uwanjani, yamefanyika pia kwenye eneo lenye milima kusini mwa Lebanon karibu na mpaka wa Israel huku vita vya Gaza vikizidi kupamba moto na kanda ya Mashariki ya Kati ikiwa katika tahadhari kwa kusubiri jibu la Israel kwa shambulizi la kombora la Iran wiki iliyopita.

Tehran imelipiza vikali baada ya Israel kuongeza mashambulizi yake nchini Lebanon, kwa lengo la kulidhoofisha kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.

Biden na Netanyahu walizungumza kuhusu mipango ya Israel katika mazungumzo kwa njia ya simu yaliyodumu dakika 30, White House ilisema.

Majadiliano hayo yalikuwa “ya moja kwa moja na yenye tija,” msemaji wa White House Karine Jean Pierre aliwaambia waandishi wa habari, huku akikiri kuwa viongozi hao wawili wanatofautiana na wako wazi kuhusu tofauti hizo.

Wawili hao wamekubaliana kuendelea kuwasiliana kwa karibu katika siku zijazo na Biden alimtaka Netanyahu kupunguza kuwadhuru raia huko Lebanon, White House ilisema baadaye.

Forum

XS
SM
MD
LG