Hafla ya kuwaidhinisha wateule wapya, inayojulikana kama consitory, itafanyika tarehe 8 Disemba, Papa huyo mwenye umri wa miaka 87 alisema wakati wa ibada ya alasiri ya kila wiki na mahujaji na watalii katika eneo la Mtakatifu Petro.
Itakuwa hafla ya 10 kuitishwa na Papa tangu kuchaguliwa kwake miaka 11 iliyopita, kama Papa wa kwanza kutoka Amerika Kusini.
Makadinali hao wapya ni kutoka nchi tofauti ikiwemo Argentina, Brazil, Chile, Peru, Italy, Uingereza, Serbia, Japan, Indonesia, Canada, Ivory Coast na Algeria.
20 kati yao wana umri wa chini ya miaka 80 na watapiga kura katika kongamano kumchagua papa mpya baada ya kifo cha Francis au kujiuzulu kwake.
Mmoja kati ya kundi hilo ana umri wa miaka 99, ni Askofu kutoka Italy. Askofu Mykola Bychok wa Kanisa Katoliki la Ukraine, ana umri wa miaka 44, atakuwa kadinali wa kwanza mwenye umri mdogo.
Forum