Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 19, 2024 Local time: 20:35

Saudi Arabia kuwekeza Misri kinyume na kutoa misaada ya kifedha


Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman.
Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman, na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, Jumanne wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji, huku wakitoa wito wa sitisho la mapigano huko Gaza na Lebanon, wakati wa mazungumzo yao mjini Cairo.

Kwa mijubu wa shirika la habari la Reuters, ziara hiyo anafanyika kukiwa na tetesi za uwekezaji mkuwa wa Saudia, nchini Misri ambayo imepokea fedha nyingi mwaka huu zikiwemo dola bilioni 35 kutoka mfuko wa UAE wa ADQ.

Ziara ya mwisho rasmi ya Mohammed Bin Salman nchini Misri ilifanyika 2022. Saudi Arabia ambayo imekuwa ikitoa misaada ya Misri katika miaka ya nyuma imeashiria kubadili mikakati na badala yake kuanza kuwekeza moja kwa moja kinyume na kutoa misaada kwa washirika wake.

Mwezi uliopita, waziri mkuu wa Misri alisema kuwa Saudi Arabia inapanga kuwekeza dola bilioni 5 nchini mwake, tofauti na fedha ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kwenye Benki kuu wa Misri. Baadhi ya uwekezaji ni pamoja na maeneo mawili ya kitalii kwenye ufukwe wa Bahari ya Shamu, pamoja na kwenye peninsula ya Sinai, yote yakiangalia upande wa pili wa Saudia Arabia.

Forum

XS
SM
MD
LG