Hali hii imekuja baada ya Congo kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Rwanda wakati mapigano kati ya waasi wanaoungwa mkono na Rwanda na majeshi ya serikali yakipamba moto kuzunguka Goma, na kuwaacha walinzi wa amani 13 na wanajeshi wa kigeni wameuawa na kuwakosesha makazi maelfu ya raia.
Kundi la waasi la M23 limepata mafanikio makubwa kwenye eneo la mpaka na Rwanda katika wiki za karibuni, na kukaribi kabisa mjini Goma, mji mkuuwa jimbo ambalo lina takriban watu milioni mbili na kituo cha kikanda cha juhudi za usalama na kibinadamu.
Watalaamu wa Congo, Marekani na Umoja wa Mataifa wanaishutumu Rwanda kwa kuwaung mkono M23, ambayo kwa kiasi kikubwa imeundwa na watu wa kabila la Watutsi ambao walijiondoa kutoka kwenye jeshi la congo zaidi ya muongo mmoja uliopita.
Ni moja ya makundi 100 yenye silaha ambayo yamekuwa yakiwania kupata udhibiti katika eneo lenye utajiri wa madini, ambako mzozo wa muda mrefu umesababisha moja ya mizozo mikubwa sana ya kibinadamu duniani.
Mapema wiki hii, waasi waliukamata mji wa Sake, uliopo kilometa 27 kutoka Goma, huku wasi wasi ukiongezeka kuwa mji huo nao haraka utaangukia kwenye mikono ya waasi.
Jeshi la Congo limesema Jumamosi kuwa limezuia uchokozi wa M23 kwa msaada wa majeshi ya ushirika, ikiwemo wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na wale kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika inayojulikana kama SAMIDRC.
Walinzi wawili wa amani wa Afrika Kusini waliuawa Ijumaa, wakati mwanajeshi wa Uruguay aliuawa Jumamosi, afisa wa UN ameliambia shirika la habari la Associated Press kwa misingi ya kutotajwa jina kwasababy hana idhini ya kuzungumzia suala hilo hadharani.
Ikiongezea, walinzi watatu wa amani kutoka Malawi waliuawa mashariki mwa Congo, Umoja wa Mataifa nchini Malawi umesema Jumamosi.
Wanajeshi saba kutoka SAMIDRC pia waliuawa wakati wa mapambano na M23 katika muda wa siku mbili zilizopita, Idara ya Ulinzi ya Afrika Kusini imesema.
Tangu mwaka 2021, serikali ya Congo na majeshi ya ushirika, ikiwemo SAMIDRC na Umoja wa Mataifa, wamekuwa wakilizuia kunid la M23 kufika mjini Goma.
MONUSCO iliingia Congo zaidi ya miongo miwili iliyopita na ilikuwa kikosi cha walinzi wa amani 14,000 katika eneo hilo.
Forum