Rwanda Jumatano ilibadili kauli kufuatia madai yake ya awali kwamba iligundua akiba yake ya kwanza ya mafuta katika Ziwa Kivu, ikisema bado iko kwenye awamu ya uchunguzi na inatafuta washirika.
Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika, CDC, pamoja na wizara ya Afya ya Rwanda, Alhamisi wamesema kuwa kesi za maambukizi ya ugonjwa wa Marburg nchini humo zimeshuka.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeishutumu Rwanda kwa kuweka vikwazo katika mazungumzo yanayoendelea kutatua mzozo wa waasi wa M23 mashariki mwa DRC ambao umesababisha zaidi ya watu milioni 1.7 kuyahama makazi yao.
Mkuu wa jeshi la Uganda, ambaye ni mtoto wa kiume wa rais Yoweri Museveni, Generali Muhoozi Kainerugaba, amesema kwamba hakuna rais atakayeongoza Uganda na kwamba hilo ni jukumu la wanajeshi au polisi.
Rwanda imemkuta na hatia mzee mwenye umri wa miaka 75 kwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya 1994, na kumuhukumu miaka 20 jela, chombo cha habari kinachoungwa mkono na serikali kiliripoti Alhamisi.
Wajumbe waliohudhulia katika kongamano la chakula na kilimo linalofanyika Kigali, Rwanda wametaja matumizi ya akili mnemba AI, kuweza kutatua changamoto zinazotokana na kilimo kwa kutafuta mbinu za kuinua kipato cha wakulima na kuongeza chakula.
Rais wa Rwanda Paul Kagame alikula kiapo Jumapili kwa muhula wa nne, akisema amani ya kikanda ni “kipaumbele chake” katika kukabiliana na mzozo unaoendelea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Nia ya Rwanda ya kulinda maslahi yake dhidi ya Uganda ndiyo chanzo kikuu cha waasi wa M23 kuzuka tena hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, makundi mawili ya utafiti yanayohusiana na Chuo Kikuu cha New York yamesema katika ripoti ya Jumanne.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano kuanzia Agosti 4 katika mkutano uliofanyika mjini Luanda chini ya upatanishi wa Rais wa Angola, ofisi ya Rais wa Angola ilisema Jumanne.
Wananchi wengi wa Rwanda wamepongeza ushindi wa kiongozi wao Paul Kagame, baadhi wakisema habidi kuondoka madarakani la sivyo nchi hiyo itatumbukia katika ghasia.
Rais Paul Kagame wa Rwanda ameshinda muhula wa nne katika uchaguzi wa urais na bunge uliofanyika Rwanda Julai 15.
Rais wa Rwanda Paul Kagame Jumamosi amekamilisha kampeni yake siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika Jumatatu.
Pandisha zaidi