Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 29, 2025 Local time: 09:06

Maafisa wa DRC walaani kuhusika kwa Rwanda katika mzozo wa M23


Picha za Rais wa Rwanda's Paul Kagame (K) na Rais wa DRC Felix Tshisekedi, Apr. 29, 2024.
Picha za Rais wa Rwanda's Paul Kagame (K) na Rais wa DRC Felix Tshisekedi, Apr. 29, 2024.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa siku ya Jumamosi, maafisa wa Congo walilaani kuhusika kwa Rwanda katika mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambako mapigano kati ya jeshi la Congo na waasi wa M23 yameongezeka.

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walioko DRC wakiondoka nchini mjini Goma, DRC Januari 25, 2025.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walioko DRC wakiondoka nchini mjini Goma, DRC Januari 25, 2025.

Kusambaa huko kumepelekea maafa miongono mwa wote walinzi wa amani na raia, mzozo unazidi kuongezeka katika kanda hiyo. Ukiongezea na gavana wa muda wa Kivu Kaskazini aliuawa na walenga shamba wakati akiwa mstari wa mbele, kwa mujibu wa Meja Jenerali Sylvain Ekenge, msemaji wa Jeshi la Congo.

Ghasia ziliongezeka mwezi huu wakati waasi wa M23 walipokamata maeneo zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali, na kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa jimbo Goma. Wakati jeshi la Congo linadai kuwa limewasukuma nyuma wapiganaji wa M23, Umoja wa Mataifa umeonya juu ya hatari ya mzozo mpana wa kikanda.

Waasi wa M23 nchini Congo.
Waasi wa M23 nchini Congo.

Waasi wa M23 wanaendelea kusonga mbele, hali ya usalama mjini Goma bado ni tete huku mamlaka zote za kieneo na jumuiya ya kimataifa zikiwa katika hali ya tahadhari kubwa. Shutuma kuwa Rwanda inawapatia waasi wanajeshi na silaha zinaendelea kuongezeka, ingawaje Rwanda imekanusha shutuma hizo.

Forum

XS
SM
MD
LG