Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 15, 2025 Local time: 17:58

Wasiwasi watanda DRC kufuatia kuuawa kwa gavana wa kijeshi


Kijana aonyesha risasi karibu na mji wa Goma, DRC. Januari 22, 2025.
Kijana aonyesha risasi karibu na mji wa Goma, DRC. Januari 22, 2025.

Hali ya wasiwasi iliendelea kutanda Jumamosi katika maeneo kadhaa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia kifo cha gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini siku ya Ijumaa.

Gavana huyo alifariki dunia kutokana na majeraha ya risasi aliyopata kwenye mstari wa mbele wa vita wakati wa mashambulizi ya waasi wa M23, jeshi lilisema.

Waasi hao wanasonga mbele kwa pande mbili karibu na mji mkuu wa j Kivu Kaskazini, Goma, katika eneo la mashariki lenye machafuko, ambapo dazani za maelfu ya watu wanakimbia na Umoja wa Mataifa unaonya kuwa ghasia hizo zinaweza kusambaa na kuwa vita vya kikanda.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana Jumatatu kujadili hali hiyo, wanadiplomasia walisema.

Meja Jenerali Peter Cirimwami Nkuba, ambaye aliongoza jimbo hilo tangu 2023, amefariki, msemaji wa jeshi Sylvain Ekenge alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Ripoti ya ndani ya Umoja wa Mataifa iliyoonekana na Reuters ilisema alijeruhiwa alipokuwa akisimamia wanajeshi kilomita 20, maili 12 kutoka Goma.

Ekenge alisema Nkuba alijeruhiwa "vitani" na kuhamishwa hadi mji mkuu Kinshasa, ambako alifariki kutokana na majeraha yake.

Hakutoa maelezo zaidi juu ya mazingira ambapo kifo cha gavana huyo kilitokea. Mapigano yamepamba moto zaidi mashariki mwa Kongo yenye utajiri mkubwa wa madini tangu mwanzoni mwa mwaka huu huku kundi linaloongozwa na Watutsi la M23 likichukua udhibiti wa maeneo mengi zaidi kuliko hapo awali.

Baada ya kuuteka mji wa Minova siku ya Jumanne, waasi hao waliteka Sake, mji mkuu wa mkoa na nyumbani kwa zaidi ya watu milioni 1, ulio karibu kilomita 20 (maili 12) magharibi mwa Goma,

Forum

XS
SM
MD
LG