Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 10:01

Rwanda yabadili kauli kuhusu madai yake ya kugundua mafuta katika Ziwa Kivu


Picha ya Ziwa Kivu, upande wa Goma DRC
Picha ya Ziwa Kivu, upande wa Goma DRC

Rwanda Jumatano ilibadili kauli kufuatia madai yake ya awali kwamba iligundua akiba yake ya kwanza ya mafuta katika Ziwa Kivu, ikisema bado iko kwenye awamu ya uchunguzi na inatafuta washirika.

Francis Kamanzi, mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Rwanda ya madini, mafuta na gesi (RMB), alikiambia awali kikao cha bunge “Habari njema ni kwamba tuna mafuta, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini humo.

Lakini bodi ya RMB baadaye ilitoa taarifa ikieleza ni mapema mnoo kuthibitisha hilo.

Ilisema uchunguzi wa pande mbili unaofuatilia mitetemeko kwenye Ziwa Kivu, ambalo inashiriki na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ulibaini “kuwepo kwa maeneo 13 tofauti ambako kunaweza kufanyika uchimbaji wa mafuta ili kuthibitisha uwepo wa mafuta.”

“RMB inawatafuta wadau wanaoweza kushiriki katika hatua zaidi za utafutaji, maendeleo na uzalishaji wa mafuta na gesi kwenye Bonde la Ziwa Kivu,” iliongeza.

Kutokana na akiba kubwa ya mafuta inayopatikana katika eneo la Maziwa Makuu na majirani Uganda na DRC, kuna uwezekano wa kupata akiba ya mafuta katika eneo la Rwanda.

Forum

XS
SM
MD
LG