Kundi hilo kuchukua udhibithi wa sehemu kubwa ya Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, ni ishara ya kuongezeka kwa mzozo mbaya katika eneo ambalo limekumbwa na miongo kadhaa ya mizozo inayohusisha makundi mengi yenye silaha.
Rwanda inasema nia yake ya msingi ni kutokomeza wapiganaji wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, lakini inatuhumiwa kujinufaisha na akiba ya madini ya eneo hilo yanayotumiwa katika soko la vifaa vya kielektroniki duniani.
“Tutaendelea kusonga mbele katika vita vya ukombozi hadi Kinshasa,” Corneille Nangaa, kiongozi wa muungano wa makundi ya waasi ikiwemo M23, aliwaambia waandishi wa habari mjini Goma.
“Tupo Goma, hatutaondoka wakati wote masuali yaliyosababisha tuchukuwe silaha yatakuwa hayajapatiwa jawabu,” alisema.
Nangaa alisema M23 itarejesha umeme na usalama mjini Goma katika siku zijazo na kuweka njia salama kusaidia watu waliotoroka makazi yao kurejea nyumbani.
Forum