Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 17:39

SADC yalaani mashambulizi ya M23 mjini Goma


Raia wakikusanyika karibu na magari ya kivita ya wanajeshi wa Afrika Kusini wa kikosi cha SADC nchini DRC, Februari 7, 2024. Picha ya AFP
Raia wakikusanyika karibu na magari ya kivita ya wanajeshi wa Afrika Kusini wa kikosi cha SADC nchini DRC, Februari 7, 2024. Picha ya AFP

Jumuia ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC imelaani “kitendo cha uvamizi cha waasi wa M23 wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC.

SADC imeongeza kwamba vitendo kama hivyo vinadhoofisha uhuru, amani na usalama wa DRC na kanda ya SADC.

“Waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda walishambulia na kuua wanajeshi 12 wa kikosi cha SADC nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ( SAMIDRC).

Katika taarifa yake, Jumuia hiyo ya kikanda imesisitiza “dhamira yake ya dhati kuendelea kuisaidia DRC katika juhudi za kulinda uhuru wake na usalama wa ardhi yake, kadhalika na amani ya kudumu, usalama na maendeleo.”

SADC inasema vitendo hivyo vya kundi la M23 vinakiuka mchakato wa amani wa Nairobi.

Hata hivyo, wizara ya mambo ya nje ya Rwanda ilisema katika taarifa, “ mzozo unaoendelea mashariki mwa DRC, hasa mapigano makali ya hivi karibuni karibu na Goma, ulichochewa na ukiukaji wa kila mara wa sitisho la mapigano uliofanywa na ushirika wa kundi la wanamgambo la FDLR, mamluki wa Ulaya, wanamgambo wa kikabila (Wazalendo), jeshi la Burundi, wanajeshi wa SAMIDRC vile vile wanajeshi wa MONUSCO.”

Mkurungenzi anayehusika na masuala ya kisiasa na usalama kwenye SADC, Kula Ishmael Theletsane amemwambia mwandishi wa VOA, idhaa ya Zimbabwe kwamba SADC ilipelekwa nchini DRC chini ya mwaliko wa serikali.

Forum

XS
SM
MD
LG