Kiongozi wa kundi la vijiji vya Djaiba katika eneo la Djugu, Jean Vianney, alisema wanamgambo wa CODECO walifanya shambulio hilo, lililoanza mwendo wa saa nane usiku, na kuwaua wakazi, na kuchoma moto nyumba zao.
“Tumehesabu watu zaidi ya 35 wamekufa asubuhi ya leo na msako unaendelea, alisema. Kiongozi wa jumuiya ya kiraia katika eneo hilo Jules Tsuba, alisema miili 49 ilikuwa imehesabiwa kufikia asubuhi ya Jumanne, na kwamba shughuli za uokoaji zilikuwa zinaendelea.
CODECO ni mojawapo ya makundi mengi ya waasi wanaopigania ardhi na rasilimali mashariki mwa Kongo.
Limeshutumiwa hapo awali na Umoja wa Mataifa kwa mashambulizi dhidi ya jamii nyingine, ikiwa ni pamoja na wafugaji wa kabila la Hema, ambayo yanaweza kuorodheshwa kama uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Wakazi wengi katika eneo la Djugu ni wa kabila la Hema.
Forum