Wanafunzi katika mji wa Bukavu walirejea shuleni, kama alivyoshuhudia mwandishi wa AFP, baada ya shule kufungwa katika mji huo siku ya Ijumaa wakati wakazi walipoanza kukimbia na maduka kufungwa kwa kohofia mashambulizi ya wapiganaji wa M23.
Waasi wa M23 ambao inasemekana wanaungwa mkono na Rwanda, katika miezi ya hivi karibuni waliteka maeneo kadhaa katika eneo hilo la mashariki mwa Congo lenye utajiri wa madini.
Mapigano yaliua maelfu ya watu na kusababisha idadi kubwa ya watu kutoroka makazi yao.
Hali kwenye uwanja wa mapigano ilikuwa shwari Jumatatu mchana baada ya mapigano makali kutokea Jumamosi kwenye umbali wa kilomita 60 kutoka Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini.
Waasi wa M23 walianza kusonga mbele kuelekea Kivu Kusini mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya kuchukua udhibiti wa mji wa Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini linalopakana na Rwanda.
Forum