Huku kila mmoja akisubiri kupata bakuli moja la chakula, wananchi wa Gaza walisema walikuwa na matumaini baada ya sitisho la mapigano kuanza kutekelezwa na kutaka misaada zaidi na uungwaji mkono kwa Gaza.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema lori 915 za misaada ziliingia Ukanda wa Gaza Jumatatu ikiwa ni siku ya pili ya kusitisha vita kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina Hamas baada ya miezi 15 ya vita.
Siku ya Jumapili, Umoja wa Mataifa ulisema baadhi ya lori za misaada 630 ziliingia katika eneo la Palestina, na angalau 300 kati yao zikienda kaskazini, ambapo wataalam wameonya kuwa kuna njaa.
Kufuatia Makubaliano ya kusitisha mapigano , eneo hilo litahitaji yanahitaji lori 600 za misaada kuruhusiwa kuingia Gaza kila siku, ikiwa ni pamoja na 50 kubeba mafuta. Nusu ya lori 600 za msaada zingewasilishwa kaskazini mwa Gaza.
Forum