Israel Jumapili ilisema ilichelewesha kuachiliwa kwa mamia ya wafungwa wa Kipalestina ambao ilikuwa imepanga kuwaachilia Jumamosi hadi pale kundi la wanamgambo la Hamas litakuwa limekidhi masharti yake.
Ofisi ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu ilisema kwamba Israel inasubiri kuwaachilia wafungwa 620 wa Kipalestina hadi Hamas itakapowaachilia mateka wengine, bila hafla ya kuwadhalilisha.
Imegusia mfano wa hivi karibuni wa mateka Hamas iliyowakabidhi, kitendo ambacho maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa kwa sababu hawakuheshimishwa.
“Mazungumzo yoyote na adui kupitia wapatanishi kuhusu hatua zozote zijazo yana masharti ya kuachiliwa kwa wafungwa 620 wa Kipalestina kama ilivyokubaliwa kwa ubadilishanaji wa miili minne na mateka sita wa Israel ambao waliachiliwa Jumamosi,” Naim, mjumbe wa kamati ya kisiasa ya Hamas aliiambia Reuters.
Forum