Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 03:00

Waconservative washinda uchaguzi nchini Ujerumani


Mgombea wa chama cha Waconservative Friedrich Merz, akihutubia wafuasi wake kwenye makao makuu ya chama, mjini Berlin, Februari 23, 2025. Picha ya AP
Mgombea wa chama cha Waconservative Friedrich Merz, akihutubia wafuasi wake kwenye makao makuu ya chama, mjini Berlin, Februari 23, 2025. Picha ya AP

Waconservative nchini Ujerumani wameshinda uchaguzi wa taifa Jumapili lakini uchaguzi huo wenye kura zilizosambaratika umekipa chama cha mrengo mkali wa kulia cha Alternative for Germany (ADF) matokeo yake mazuri kwa kupata nafasi ya pili.

Kiongozi wa mrengo wa kikiconservative wa kushoto Friedrich Merz anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuanzisha mazungumzo ya kuunda serikali ya ushirika.

Merz, ambaye haana uzoefu katika masuala ya utawala, anatarajiwa kuwa Kansela wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Ulaya unaodorora, jamii yake ikigawanyika kuhusu suala la uhamiaji na usalama wake ambao umejikuta katika malumbano na Marekani na Russia na China zenye msimamo mmoja.

Baada ya muungano wa Kansela Olaf Scholz kusambaratika, Merz mwenye umri wa miaka 69 lazima aunde serikali ya ushirika kutoka bunge lililogawanyika na mchakato huo unaweza kuchukua miezi kadhaa.

Merz aliikosoa Marekani kwa matamshi makali baada ya ushindi wake, akikemea matamshi “ ya kutisha yaliyotumiwa na Washington wakati wa kampeni, akiyalinganisha na uingiliaji kati wa uvamizi wa Russia.

Merz ameikosoa vikali Marekani licha ya Rais Donald Trump kupongeza ushindi wa Waconservative.

“Kama vile Marekani, wananchi wa Ujerumani wamechoshwa na ajenda isiyoeleweka, hasa kuhusu nishati na uhamiaji, ambayo imekuwepo kwa miaka mingi,” Trump aliandika kwenye mtandao wake wa Truth Social.

Forum

XS
SM
MD
LG