Taarifa hiyo imeongeza kusema kuwa “ Waziri Rubio na Waziri wa Mambo ya Nje Antonio wamejadili kuhusu mchakato wa Luanda na uongozi wa Angola kufanyakazi kutafuta suluhisho la amani kwa mzozo wa mashariki mwa DRC.”
Hata hivyo Washington imeonya kuhusu uwezekano wa kuweka vikwazo dhidi ya maafisa wa Rwanda na Congo kutokana na mzozo huo.
Kuhusu waraka wa kidiplomasia ambao Reuters imeuona mapema mwezi huu , Marekani ilisema kwamba utulivu katika eneo unataka jeshi la Rwanda kuondoa vikosi vyake na silaha za hali ya juu kutoka DRC.
Forum