Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 16:21

Guterres asema dola la DRC liheshimiwe


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Jumamosi amesema dola ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iheshimiwe na kuepusha vita vya kikanda, katika mkutano wa Umoja wa Afrika, siku moja baada ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda kuuteka mji mkuu wa pili wa jimbo la DRC.

Huku shinikizo la kimataifa likiongezeka kwa Rwanda kuzuia mapigano mashariki mwa DRC, mzozo huo ulitarajiwa kugubika mkutano uliofunguliwa mjini Addis Ababa.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, alionekana akihudhuria mikutano katika mkutano huo, lakini rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, hakuwepo katika mkutano huo wakati waasi wa M23 wakisonga mbele katika ardhi ya nchi yake.

Baada ya kulitimua jeshi la Congo na kuteka Goma, Kivu Kaskazini mwezi uliopita, waasi wanaoungwa mkono na Rwanda walisonga kwenda Kivu Kusini.

Forum

XS
SM
MD
LG