Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 15:57

EU inatafakari hatua za kunusuru DRC


Umoja wa Ulaya, (EU) Jumamosi umesema unatakari kwa dharura njia za kukabiliana na ongezeko la mashambulizi ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya vikosi vinavyoungwa mkono na Rwanda kuuteka mji mkubwa wa pili.

Wakiwa wameushateka Goma mwezi uliopita, waasi wa M23 wamesonga mbele kusini na kushikilia uwanja wa ndege muhimu kabla ya kuandamana bila upinzani Ijumaa katika mji muhimu wa Bukavu, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama na kibinadamu.

“Nimeshtushwa na habari za vikosi vya M23 vinavyoungwa mkono na Rwanda kuuteka uwanja wa ndege wa Kavumu na kuingia Bukavu, na kupuuza wito wa kimataifa wa kusitisha mapigano,” msemaji wa Tume ya Ulaya, Anouar El Anouni aliandika kwenye mtandao wa X.

EU kwa haraka inasema inatafakari njia zinazoweza kutumika dhidi ya harakati za M23.

Forum

XS
SM
MD
LG