Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 06, 2025 Local time: 11:21

UN: Watoto wauawa na M23 huko Bukavu, Congo


Ravina Shamdasani, Msemaji wa ofisi ya Haki za Binadamu ya UN.
Ravina Shamdasani, Msemaji wa ofisi ya Haki za Binadamu ya UN.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wamewaua watoto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ofisi ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa imeonya kwamba hali inaendelea kuwa mbaya mashariki mwa DRC na kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Msemaji wa ofisi hiyo Ravina Shamdasani, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba wana uthibithisho kwamba kuwa kuna baadhi ya watoto walikuwa na silaha.

Waasi wa M23 na wanajeshi wa Rwanda wamedhithi miji ya Goma na Bukavu.

Shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, limesema kwamba zaidi ya watu 150,000 wamekimbia makwao, Kivu kusini.

Wataalam wa umoja wa mataifa wanasema kwamba Rwanda inaliongoza kundi la M23 wanaosaidiwa na wanajeshi wa Rwanda wasiopungua 4000.

Serikali ya DRC imeishutumu Rwanda kwa njama za kuchukua sehemu ya DRC, huku ikiiba madini yake.

Forum

XS
SM
MD
LG