Hapakuwa maelezo ya moja kwa moja kutoka serikali ya Congo, ambayo imekuwa ikipinga mara kwa mara kufanya mazungumzo na M23.
Taifa hilo la kusini mwa Afrika limekuwa likijaribu kuwa mpatanishi ili kufikia sitisho la mapigano la kudumu na kupunguza mvutano kati ya Congo na jirani yake Rwanda, ambayo imekuwa ikituhumiwa kuwaunga mkono M23.
Rwanda inakanusha kutoa silaha na wanajeshi kwa waasi wa M23, na inasema kile jeshi lake inachofanya ni kujihami dhidi ya jeshi la Congo na wanamgambo wenye nia mbaya dhidi ya Kigali.
Waasi wa M23 waliteka miji mikubwa ya mashariki mwa Congo tangu mwezi Januari.
Rais wa DRC Felix Tshisekedi alifanya ziara ya kikazi mjini Luanda na alikutana na mwenzie Joao Lourenco, ofisi ya rais wa Angola ilisema katika taarifa kwenye Facebook.
“Angola kama mpatanishi katika mzozo wa mashariki mwa Congo, itaanzisha mawasiliano na M23, ili wajumbe kutoka Congo na M23 wafanye mazungumzo ya moja kwa moja mjini Luanda katika siku zijazo,” ofisi ya rais iliongeza.
Forum