Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 11, 2025 Local time: 02:10

Mgonjwa wa pili wa Ebola afariki dunia nchini Uganda


Daktari wa Uganda akimpa chanjo mtu aliyewasiliana na mgonjwa wa Ebola, mjini Kampala
Daktari wa Uganda akimpa chanjo mtu aliyewasiliana na mgonjwa wa Ebola, mjini Kampala

Mgonjwa wa pili wa Ebola, mtoto mwenye umri wa miaka minne alifariki nchini Uganda, shirika la afya duniani (WHO) lilisema, likinukuu wizara ya afya ya nchi hiyo. Kufuatia kifo hicho, idadi ya visa vya Ebola vilivyothibitishwa sasa ni 10.

Taifa hilo la Afrika Mashariki lilitangaza mlipuko wa ugonjwa huo unaoambukiza sana na kusababisha vifo kutokana na kuvuja damu mwezi Januari baada ya kifo cha muuguzi mwanaume katika Hospitali kuu ya Mulago jijini Kampala.

Ofisi ya WHO nchini Uganda iliandika kwenye mtandao wa X siku ya Jumamosi kwamba wizara ya afya iliripoti kisa kipya cha Ebola katika hospitali ya Mulago cha mtoto wa miaka minne, ambaye alifariki dunia siku ya Jumanne.

Mulago ndiyo hospitali pekee ya taifa inayoshughulikia visa vya Ebola.

Wizara ya afya ya Uganda ilisema tarehe 18 Februari kwamba wagonjwa wote wanane wa Ebola ambao walikuwa wanapewa matibabu waliondoka hospitali lakini watu 265 waliowasiliana nao bado wamewekwa karantini mjini Kampala na katika miji mingine miwili.

Dalili za Ebola ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa na misuli. Virusi hivyo huambukiza kwa kugusa majimaji ya mwili yaliyoambukizwa na viungo vingine vya mwili.

Forum

XS
SM
MD
LG