Uganda ilitangaza ugonjwa huo hatari kuwa janga Januari, kwenye mji mkuu wa Kampala kufuatia kifo cha muuguzi mwanamme kwenye hospitali kuu nchini humo. Mgonjwa wa pili aliyefariki ni mtoto wa umri wa miaka minne kulingana na Shirika la Afya Duniani, WHO, likitaja wizara ya Afya ya Uganda.
Ngashi Ngongo ambaye ni afisa wa CDC aliwaambia wanahabari kwamba baada ya kutoa taarifa za hali Alhamisi, tayari kesi tatu za maambukizi zimeripotiwa wakati nyingine mbili zikisubiriwa kuthibitishwa. Ngongo aliongeza kusema kwamba wilaya mbili mpya zimeripoti kesi za Ebola na kwamba kwa ujumla Uganda imeripoti kesi 14 za maambukizi na vifo viwili tangu kuzuka kwa ugonjwa huo, kulingana na CDC.
Ugonjwa unaofanana na Ebola wa Marburg uliripotiwa kwenye nchi Jirani ya Tanzania Januari mwaka huu.
Forum