Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 07:06

Azimio la Marekani kuhusu kumaliza vita vya Ukraine lapitishwa na Baraza la usalama la UN


Mabalozi wakipigia kura azimio la kuthibitisha tena uhuru wa Ukraine, katika kikao cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Februari 24, 2025. Picha ya AFP.
Mabalozi wakipigia kura azimio la kuthibitisha tena uhuru wa Ukraine, katika kikao cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Februari 24, 2025. Picha ya AFP.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu lilipitisha azimio lilioandikwa na Marekani siku ya kumbukumbu ya miaka mitatu ya uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine, azimio ambalo linachukua msimamo wa kutoegemea upande wowote katika mzozo huo.

Ni wakati Rais wa Marekani Donald Trump akifanya juhudi za kufikia amani.

Kufikia sasa, Baraza hilo lenye wanachama 15 lilikuwa limeshindwa kuchukua hatua yoyote kuhusu mzozo wa Ukraine kwa sababu Russia ina kura ya turufu.

Azimio la MareKani lilipata kura 10 za kuliunga mkono, huku Ufaransa, Uingereza, Denmark, Ugiriki na Slovenia zikijizuia kutoa msimamo.

“Azimio hili linatuweka kwenye njia ya amani. Ni hatua ya kwanza, lakini muhimu, ambayo sote tunapaswa kujivunia,” kaimu Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Dorothy Shea aliliambia Bazara hilo.

“Sasa ni lazima tuitumie kujenga mustakabali wa amani kwa Ukraine, Russia na Jumuia ya Kimataifa.”

Forum

XS
SM
MD
LG