Chama cha Waliberal kimemtangaza Carney kama mrithi wa Trudeau Jumapili baada ya wanachama kumpigia kura katika uchaguzi wenye ushindani.
Trudeau alijuzulu mwezi Januari kufuatia umaarufu katika utendaji kazi wake kushuka sana baada ya karibu muongo mmoja akiwa madarakani.
Carney mwenye umri wa miaka 59 sio mwanasiasa na hajawahi kuwa na wadhifa wowote serikalini, jambo ambalo kwa kawaida lingemuondoa kwenye kinyang’anyiro nchini Canada. Lakini kujitenga kwake na Trudeau na wasifu wake kama mfanyakazi wa benki wa muda mrefu kulimsaidia, na Carney amedai kuwa yeye ndiye mtu pekee aliye tayari kumdhibiti Trump.
Forum