Rwanda inakabiliwa na shinikizo la kimataifa kutokana na madai kwamba inaunga mkono kundi la M23 ambalo tangu mwezi Januari mwaka huu, limeteka maeneo ya mashariki mwa Kongo ikiwa ni pamoja na miji ya Goma na Bukavu, pamoja na madini ya thamani.
Kigali inakanusha kuunga mkono kundi hilo lakini inasema wanajeshi wake wanajilinda dhidi ya makundi hasimu yaliyo nchini Kongo.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Uingereza imesema hadi pale kutakapopatikana mafanikio makubwa katika kumaliza uhasama na kuondolewa kwa Vikosi vyote vya Ulinzi vya Rwanda katika ardhi ya Kongo, Uingereza itachukua hatua.
Hii itajumuisha kutohudhuria vikao vya ngazi ya juu vinavyoandaliwa na serikali ya Rwanda; kupunguza shughuli za uhamasishaji wa biashara na Rwanda; na kusitisha misaada ya moja kwa moja ya fedha baina ya nchi mbili kwa serikali ya Rwanda, bila kujumuisha msaada kwa watu maskini, walio hatarini zaidi.
Forum