Mwakilishi wa shirika la kuhudumia wakimbizi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi Brigitte Mukanga-eno, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba mapema wiki hii zaidi ya watu elfu 9 walivuka mpaka kutoka DRC na kuingia Burundi.
Kundi la wanamgambo wa M23 wameongeza operesheni zao kwa zaidi ya muongo mmoja wa mzozo wa mashariki mwa DRC.
Rwanda imeshutumiwa na jumuiya ya kimataifa mara nyingi kulisaidia kundi la wanamgambo wa M23 lakini imekanusha.
Maeneo kadhaa kaskazini magharibi mwa Burundi watu wamejaa wengine wamekoseshwa makazi mara kadhaa na wamewasili wakiwa wamejeruhiwa au wana matatizo ya afya kama vile Surua, hiyo ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Mukanga -eno amesema watu elfu 36 wamekimbilia Burundi wengine wakitumia mitumbwi kuvuka ziwa Rusizi ambalo linatengenanisha nchi hizo mbili, wakati wengine elfu sita wameingia kupitia mpaka rasmi wa Bujumbura kuanzia Februari 14.
UNHCR inatarajia kuwahamisha watu waliokoseshwa makazi ambao wamehifadhiwa kwa muda katika uwanja wa michezo ulio wazi pamoja na shule na makanisa katika eneo la ardhi ambalo huduma za kibinadamu zinaweza kutolewa .
Forum