Mzozo huo sio tu kutokana na kusonga mbele kwa kundi la waasi la M23 ambalo inasemekana linaungwa mkono na Rwanda au mvutano kati ya Kinshasa na Kigali, Kabila aliandika katika makala ya maoni kwenye gazeti la Afrika Kusini la Sunday Times.
Wapiganaji wa M23 waliteka maeneo kadhaa kwa haraka katika wiki zilizopita na hadi sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya mashariki mwa DRC yenye utajiri wa rasilimali, huku kukiwa na hofu kwamba mzozo huo unaweza kuvuka mipaka.
Tangu Tshisekedi aingie madarakani mwaka wa 2019 baada ya kushinda uchaguzi wa 2018, hali nchini DRC imezidi kuzorota hadi kufikia kwenye hatua ya mpasuko,” Kabila aliandika.
Uchaguzi wa Disemba 2023 ambao ulimpa Tshisekedi muhula wa pili kwa kishindo ulikuwa wenye “udanganyifu”, alisema, akiishtumu serikali kwa kukandamiza upinzani wa kisiasa na rais kuwa “dikteta.”
“Vitisho, watu kukamatwa kinyume cha sheria, mauaji ya kiholela, pamoja na kutimuliwa kwa wanasiasa, waandishi wa habari na viongozi wa mashirika ya kiraia, wakiwemo viongozi wa makanisa, ni miongoni mwa sifa za utawala wa Tshisekedi,” alisema.
Forum