Wapiganaji wa M23 walichukua udhibiti wa Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini wiki iliyopita, baada ya kuuteka mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini wa Goma mwishoni mwa mwezi uliopita.
“Hali ya usalama mashariki mwa DRC imefikia viwango vya kutisha, “ waziri mkuu Judith Suminwa Tuluka aliliambia Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu mjini Geneva, akisema tangu Januari, “ vifo vya zaidi ya wananchi wetu 7,000” viliripotiwa.
AFP haikuweza kuthibitisha idadi hiyo.
Forum